Kuna uwezekano ya kuwa wengi hawamufahamu Seven Mosha kama vile wanavyofahamika wasanii anaowasimamia kazi zao za muziki.
Jumapili,
Feb 5, 2017 akiongea na kitengo cha Buzz kwenye gazeti kuu nchini Kenya
la Nation, Mosha alieleza kuwa alikuwa mtangazaji katika kituo cha
redio cha Clouds FM na pia kituo hicho kilipoanzisha label ya kurekodi
maarufu kama Smooth Vibe, alikuwa mhusika mkuu katika masuala ya
kusikiliza na kuandika muziki.
Alitoka
Clouds FM mwaka wa 2009 na akajiunga na kituo cha televisheni cha MTV
ambapo anasema alihudumu kwa takribani miaka mitano toka 2005-2010
ambapo alikuwa katika kitengo cha ( Artiste and Repertoire) maarufu kama
A&R. Pia Seven alihudumu katika kampuni kubwa ya muziki duniani ya
Sony kwa muda kabla ya kusimamia tawi la Rockstar4000.
Seven
Mosha anasema alizaliwa Nairobi Kenya lakini akahamia Moshi, Tanzania.
Familia yake ambayo iliishi katika mtaa wa kifahari wa Lavington jijini
Nairobi, ilihamia Tanzania akiwa na umri wa miaka minne tu. Jina lake la
kuzaliwa ni Christine Mosha lakini baada ya kufundishwa kuhusu maajabu
saba ya ulimwengu na dhambi saba kuu katika dunia basi nambari saba
”Seven” ikawa nambari yenye nguvu katika maisha yake na ndio maana
akajiita Seven kama aka yake.
Aliliambia
gazeti hilo kuwa, haamini kama anaitwa Christine, maana kama angalikuwa
na chembechembe za hulka la jina Christine, marafiki zake wangelikuwa
Elizabeth ama Victoria ambao wengi wao huwa wanategemea mabwana zao
kuwafanyia kila kitu katika maisha ilhali wakibaki kufanya kazi za
nyumbani kwa kimombo ”Housewives.”. Ni kilinukuu gazeti hilo, (She
does not believe she is a Christine,if she had a Christine character
her friends would be called Elizabeth or Victoria and she would a
housewife and stay at home).
Akigusia
ushindani uliopo kati ya Diamond na Alikiba, Mosha aliliambia gazeti
hilo kuwa, anaamini ushindani katika tasnia ya burudani ya muziki ni
mzuri, kwasababu inawapa wasanii motisha ya kuvalia njuga kazi zao na
kutoa vitu venye ubora wa hali ya juu na kuuikuza sanaa ya Afrika
Mashariki katika viwango vya dunia.
Lakini
akaongezea kuwa ataunga mkono ushindani kama huo pekee, pale ambapo
hautahatarisha maisha ya masanii yeyote yule. Bali anafurahia vile
Diamond na Alikiba wanavyoshinda kutoka production ya muziki hadi kwa
style za kimaisha.
Mosha
aliongezea kuwa, huu ni mwaka wake wa sita tangu aanze kufanya kazi na
Alikiba. Na walikutana kwa mara ya kwanza katika project ya One8 ambapo
katika project hiyo aliwasimamia wasanii wa Afrika Mashariki na
alisisitiza kuwa alipenda kila kitu kuhusu Alikiba. Baada ya project ya
One8 kuisha walikuwa wakiwasiliana na mwisho wakaamua kufanya kazi
pamoja. Pia Seven ni rafiki mkubwa wa Lady Jaydee, na picha ya macho
yake ndio yalikuwa kwenye cover ya album ya kwanza ya Lady Jaydee
”Machozi”.
Mkali
wa Yahaya, Jide baada ya kutalakiana na mume wake ambaye pia alikuwa
manaja wake, Gardiner G Habash, alimuomba Mosha kusimamia kazi zake za
muziki na akakubali. Baadaye akakutana na Baraka The Prince katika
uzinduzi wa wimbi wa Alikiba, akamuuliza kama angekubali kusimamia kazi
zake na Baraka hakusita kukubali.
Gazeti
la Daily Nation, linamuita malkia wa marejeo au kwa lugha ya kizungu (
Queen of comebacks). Hii ni kwasababu ya uwezo wake aliouonyesha,
kuwarudisha kwenye game Alikiba akiwa na hit Mwana na Jaydee ambaye
alirudi kwenye muziki kipindi ambacho nyimbo zake zilikuwa hazipati air
play kwenye kituo cha redio cha Clouds FM ambacho ni muhimu sana kwenye
ku-support wanamuziki wengi nchini Tanzania kwasababu za tofauti za
kibinafsi ambayo baadaye ilitatuliwa.
Anasema
hutumia pesa zake kwa kusafiri nchi tofauti tofauti za dunia, na kila
mwaka huenda nchi tatu tofauti ambazo huwa ni geni kwake. Anapenda
kupika na anapenda chakula kizuri pia.
0 comments:
Post a Comment