Friday, February 17, 2017

 
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange amezindua rasmi mashindano ya kuadhimisha Miaka 10 ya Klabu ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi ya Lugalo.
 
Mara baada ya kuzindua mashindano hayo Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange amewasifu wanachama wa klabu hiyo kwa kuweza kutimiza miaka 10 kwani si jambo jepesi kwa klabu kudumu na kuzidi kuwa na kiwango maridadi.
 
 
"Ninayo furaha kuwapongeza wanachama wa klabu hii kwa kufikisha miaka 10. Naupongeza uongozi wa klabu hii kwani naelewa klabu haiwezi kuwa hai bila ya wanachama walio hai" amesema
Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyange.
 
Katika hatua nyingine Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Davis Mwamunyangeamewataka wananchi wa kawaida kujitokeza kwa wingi katika kuutumia uwanja wa gofu lugalo kwani ni mali yao pia na si mali ya jeshi pekee.
 
 
Mashindano haya yatafanyika kwa siku tatu katika viwanja vya Lugalo Gofu Lugalo, kuanzia tarehe 17 hadi 19 februari 2017 yakiwashirikisha wachezaji wa kulipwa (Pros), wachezaji wasaidizi (Caddies) na wachezaji wa Ridhaa (Armatures
 
 
 
 

0 comments:

Post a Comment