Wednesday, February 1, 2017

Msanii wa bongo fleva Dayna Nyange ambaye kwa sasa anafanya vizuri na chupa aliloliachia kwa kushtukiza akiwa amemshirikisha Billnass “Komela”.

Dayna Nyange amefunguka na kuwasihi wasanii wa kike nchini kujifunza kuandika nyimbo zao wenyewe ili kuweza kupata ‘melodi’ na mizuka ya kuimba nyimbo nzuri.
16122793_195734467561099_8513337367854055424_n
Dayna Nyange
Dayna adai, “siyo vibaya kuandikiwa wimbo lakini kwa wakati mwingine ni vizuri kujua kujiandikia mwenyewe kwani unaweza kupata zali la kuingia studio kubwa hata nje ya nchi na kupata nafasi ya kurekodi hata na wasanii wakubwa ukashindwa na ukapoteza zali kwa kuwa hujui kuandika”. Alisema kwenye eNewz
Pia Dayna hakusita kumwagia sifa msanii mwenzake Maua Sama kwani anadai aliwahi kusikia kuwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanaoweza kujiandikia nyimbo na kumsifia kwamba ni mwandishi mzuri.
Mbali na hilo, Dayna kachaguliwa kuwania tuzo za BAE Awards 2017 za nchini Nigeria akiwa ni msanii pekee kutoka Tanzania.
Hitmaker huyo wa Komela amechaguliwa katika vipengele viwili ikiwemo kimoja cha BEST AFRICAN ACT akichuana na Eddy Kenzo (Uganda), King Kaka (Kenya), Stoneboy (Ghana), Jah Vinci (Jamaica).
Kipengele kingine anachowania ni BEST VOCAL PERFORMANCE FEMALE kupitia wimbo wake ‘Angejua’ ambapo anawania tuzo hiyo na Aramide, Ngowari na Rocknana (wote kutoka Nigeria).

0 comments:

Post a Comment