
KIZUNG-UMZIA
ishu ‘inayo-trend’ kwa sasa kwenye burudani hususan katika Muziki wa
Bongo Fleva bila kupapasa utataja ishu ya msanii chipukizi aliyejizolea
umaarufu wa ghafla, Athuman Omary ‘Harmorapa’.
Harmorapa
amejizolea umaarufu kutokana na kuhusishwa kufanana muonekano na staa
wa muziki huo ambaye ni mmoja kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB),
Rajab Abdulhan ‘Harmonize’. Licha ya kuhusishwa huko, pia jina lake lina
ukaribu na Harmonize ila utofauti wa hao wawili, Harmorapa anafanya
Muziki wa Hip Hop wakati mwenzake anaimba.
Kimuziki
Harmorapa
amefahamika wiki tatu zilizopita kupitia ngoma yake ya Usigawe Pasi
ambapo katika video ya ngoma hiyo amemtumia dada anayefananishwa
kimuonekano na muigizaji kutoka Bongo Muvi, Jacqueline Wolper. Ikumbukwe
kuwa Wolper yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Harmonize.
Tangu
kufahamika kwa dogo huyo ambaye anatokea mkoani Mtwara kama ilivyo kwa
Harmonize, mashabiki wengi wa muziki wamekuwa wakimuongelea na wengine
kumfuatilia kwa ukaribu.
Kushika mkwanja
Moja
ya matukio ambayo yamewashtua wengi ni kitendo cha kuonekana na
‘maburungutu’ ya pesa ‘mkwanja’ jambo ambalo limewahi kufanywa na
wanamuziki wengine hivi karibuni kama vile Nay wa Mitego na Rayvanny.
Itakumbukwa
kuwa, baada ya picha za Nay akiwa amekumbatia maburungutu ya pesa
kusambaa mitandaoni, alifanyiwa mahojiano katika kipindi kimoja cha TV,
juu ya utajiri wake huo na kusema kuwa biashara pamoja na muziki wake ni
vitu vinavyomwingizia pesa nyingi.
Alisema mali zake na kila kitu zinafika bilioni, ukichanganya hela zilizo benki pamoja na biashara anazofanya thamani yake.
Kwa
upande wa Harmorapa kwake ameonesha kumbe inawezekana kushika pesa hizo
ndani ya muda mfupi. Hivi karibuni naye aliachia picha kibao
zikimuonesha akiwa na maburungutu ya pesa.
Swali
ni je, pesa hizo ni zake alizozipata ndani ya kipindi kifupi tangu
aingie kwenye muziki au kachukua tu ili apigie picha na kutafuta kiki?
Kama kafanya kwa lengo la kiki, tuna-wezaje kuamini kwamba zile
walizopigia picha akina Nay wa Mitego ni zao? Jibu utakuwa nalo wewe
msomaji?
Kumi-liki gari
Licha
ya kuonesha mkwanja huo, Harmorapa pia anadaiwa kuzawadiwa mkoko aina
ya Nissan Murano na meneja wake ambapo jambo kama hilo limeshawahi
kutokea kwa wasanii wengi wa muziki wa Bongo Fleva kukabidhiwa mkoko na
mameneja wao kama vile Rayvanny, Queen Darleen na Dogo Janja.
Katika
hili nalo bado kuna siri nyuma ya pazia! Hivi kweli gari hilo kapewa au
nalo kaomba apigie picha? Maana alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha
TV hivi karibuni, dogo huyo alionekana kutuna kabisa kwenye usukani wa
gari hilo kuonesha ni lake lakini baadaye kuna picha kapiga yuko kwenye
siti ya abiria.
Kubadili wana-wake
Alipoanza
kuonekana kwenye video alikuwa na Wolper Feki na hata katika
‘interview’ mbalimbali za TV na redio alizokuwa akifanyiwa alikuwa
akiongozana na Wolper huyo.
Lakini
kwa siku za hivi karibuni alimtambulisha mwanamke mwingine kuwa ndiye
aliyenaye baada ya kumpiga chini Wolper Feki. Mwanamke wake mpya ni
video queen ambaye yupo katika Video ya Too Much ya Darassa.
Kwa
anachokifanya Harmorapa ndani ya muda mfupi kubadili wanawake, ni jambo
ambalo wasanii wengi nao wamekuwa wakifanya hivi katika uhusiano wao
akiwemo Nay ambaye alishawahi kutoka na Shamsa Ford, Siwema na pia
akadaiwa kutoka na Pam D.
Ndiyo
maana naweza kusema kuwa, anachokifanya Harmorapa ndicho wanachokifanya
wasanii walio wengi na kwa hili niseme tu kwamba ni ulimbukeni!
0 comments:
Post a Comment