Huwezi kuwataja mastaa wa muziki ambao wanaingiza pesa ndefu sana tofauti na kazi ya muziki ambayo wanafanya ukaacha kumtaja Juma Jux, kwasababu ni mmoja kati ya watu ambao wanamiliki brands kubwa sana za mavazi hapa Bongo.
Jux ameiambia Perfect255 kuwa brand yake ya African Boy inamuingizia mkwanja mrefu sana hata kuzidi kazi ya muziki ambayo anaifanya.
Japo kuwa zote zinategemeana lakini Jux amefunguka kuwa African Boy ni mchongo ambao unampatia pesa za kila siku tofauti na muziki ambao ni mpaka apate show.
“African Boy ni kitu ambacho kinaniingizia pesa sana, hata muziki pia unaniingizia pesa lakini ni kwa muda mpaka nipate shows. Kuna muda shows zinaweza zisije, kiasi kwamba ndani ya mwezi ukafanya shows 2 tu. Japo kwenye show inakuja pesa nyingi kwa wakati mmoja lakini African Boy ni pesa ya kila siku.” Alisema Jux.
Hayo ni baadhi tu kati ya mengi ambayo Jux amefunguka juu ya brand yake ya African Boy, play video hii hapa chini kumsikiliza Jux akifunguka juu ya mchongo huo.
0 comments:
Post a Comment