Hakuna furaha duniani kama kuona wakongwe wanakubali kitu unachokifanya kwenye fani ambayo umewakuta.
Hii inaweza ikawa good news kwa msanii zao la jumba la vipaji Bongo( THT),Maua Sama, baada ya Cassim Mganga kutamka wazi kwenye mahojiano na kipindi cha Supermega kinachoongozwa na Prince Ramalove kupitia Kings Fm kuwa anapenda sana anachokifanya Maua Sama.
Cassim amefunguka hayo wakati akijibu swali langu la sababu ya yeye kuweka caller tune(muito)Sisikii ya Maua Sama.
“Napenda sana kumsikiliza Maua Sama,” alisema Cassim. “Ni mwanamuziki hodari sana, anajua kuimba. Huenda mbeleni huko natarajia kufanya naye chochote,” aliongeza.
Cassim Mganga kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya Somo aliyomshirikisha mkongwe Nyota na Bendi nzima ya Kilimanjaro.
0 comments:
Post a Comment