Tuesday, February 28, 2017

Moja kati ya vitu ambavyo viliteka hisia za watu wengi sana hapa Bongo weekend iliyopita ni pamoja na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara aliowakutanisha watani wa jadi yaani SIMBA na YANGA katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.

Ni watu wengi ambao walihudhuria mchezo huo ikiwa ni viongozi mbali mbali wa serikali, watu maarufu kama Mwana FAWema SepetuOmmy Dimpoz bila kumsahau hitmaker wa ngoma ya Hela Madee.
Shilawadu wamezipenyeza taarifa hadi kwa mwakilishi wao Soudy Brown kumuhusu Madee kuchezeshewa virungu na askari wa usalama waliokuwepo uwanjani hapo siku ya mchezo.
Soudy Brown amemvutia waya Madee na kumuuliza ukweli kuhusiana na suala hilo na uhondo kamili nimekuwekea kwenye video hii hapa chini. Bonyeza play kusikiliza mazungumzo yao intro to outro.

0 comments:

Post a Comment