Monday, February 20, 2017


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amemuunga mkono sera ya Rais wa Marekani Donald Trump kwamba "Marekani iwe ya Wamarekani".


Hii ni mara ya kwanza kwa Bw Mugabe, kumzungumzia Bw Trump, na amesema alishangazwa na ushindi wa kiongozi huyo wa Republican.

" Donald Trump anazungumzia uzalendo, Marekani iwe ya Wamarekani - katika hilo, nakubaliana naye. Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe," amesema Mugabe.
Rais wa Marekani, Donald Trump.




Mahojiano kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 tangu kuzaliwa kwake.


Katika hatua nyingine Rais Mugabe ameongoza Zimbabwe nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1980 amesema anafaa kuendelea kuliongoza taifa hilo.

0 comments:

Post a Comment