Mwanadada
Maria Sharapova amepata mwaliko wa kushiriki katika michuano ya wazi ya Madrid ikiwa
yamesalia majuma mawili kabla hajamaliza adhabu yake ya kukaa nje ya uwanja kwa
miezi 15.
Sharapova
alifungiwa mara baada ya kubainika kwamba ametumia dawa aina ya meldonium, dawa ambayo imepigwa marufuku kutumika michezoni.
Mara
baada ya kupewa kadi ya mwaliko wa kushiriki ni wazi sasa Sharapova ataonekana
tena katika ulimwengu wa mchezo wa tennis tarehe 5 ya mwezi May.
Mratibu
wa tamasha hilo Manolo Santana amesema wamelazimika kumualika Sharapova kwani
alionesha nia ya kutaka kushiriki katika michuano hiyo.
Manola
amesema Sharapova amekuwa mchezaji bora
kwa zaidi ya miaka 15 lakini pia amekuwa akifanya vema katika michuano ya wazi
ya Madrid kutokana na uwezo alionao.


0 comments:
Post a Comment