Mbunge wa
Simanjiro, Mh James Ole Millya ametoa pongezi kwa viongozi wa serikali
ya awamu ya tano kutokana na namna ambavyo imekuwa ikiwajali na kuwahudumia wananchi.
Akizungumza kwenye mikutano miwili ya
hadhara iliyofanyika Orkesumet na Mererani wilayani Simanjiro, Manyara, James Ole Millya amesema viongozi wa serikali ni wachapakazi wakiongozwa vema na Waziri Mkuu Mh. Kassim Majaliwa .
“Serikali
hii ina viongozi wachapakazi akiwemo Waziri Mkuu. Kwa mara ya kwanza katika
jimbo hili, wananchi watapata maji safi kupitia mradi wa maji kutoka mto Ruvu
unaoendelea kujengwa hivi sasa,” amesema kwenye mkutano wa hadhara wa
Orkesumet.
Alitumia
fursa hiyo kumuomba Waziri Mkuu afuatilie suala la ujenzi wa hospitali ya
wilaya kwani sasa hivi wanategemeakituo cha afya na hali ikibadlika inabidi
mgonjwa apeekewe Arusha mjini ambako ni umbali wa km. 150 kutoka Orkesumet
yalipo makao makuu ya wilaya hiyo.
Pia aliomba
ijengwe barabara ya lami ya kuunganisha wilaya hiyo pamoja wilaya jirani za Hai
na Kiteto.
Akiwa
Mererani, Bw. Ole Millya aliipongeza Serikali kwa kujenga barabra ya lami
kutoka uwanaja wa ndege wa KIA hadi Mererani. Hata hivyo, aliiomba serikali
iongeze juhudi ili barabara hiyo iweze Mererani na Orkesumet.
Akihibu
hoja hizo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimpongeza mbunge huyo kwa uungwana
wake wa kutambua juhudi ambazo Serikali imezifanya kwa wananchi wa jimbo lake.
Waziri Mkuu
ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara, aliwaambia
wakazi hao kwamba Serikali itaendelea kufanya nao kazi bila kumbagua mtu yeyote
kwa sababu ya itikadi za kisiasa.
“Mmempa
yeye dhamana ya kuwawakilisha kama mbunge wenu lakini dhamana ya kuongoza nchi
mmempa Mheshimiwa Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuwapigia kura. Kwa hiyo,
kazi yetu ni kuwatumikia ili tutatue kero zinazowakabili wana-Simanjiro,”
alisema.
Akizungumzia
sekta ya afya, Waziri Mkuu alisema kituo cha afya cha Orkesumet kimepokea sh.
milioni 49 kati ya sh. milioni 57 zilizoombwa ili kukiimarisha katika utoaji wa
huduma za tiba.
“Tumeshatuma
fedha nyingine sh. milioni 163 kati ya sh. milioni 190 zilizoombwa ili
kununulia dawa, vifaa tiba na vitendanishi. Pia kun ash, milioni 483 zimetengwa
kwa ajili ya kuimarisha huduma za afya vijijini,” alisema.
“Nia yetu
ni kujenga hospitali kubwa ya wilaya lakini ni lazima tuimarishe miundombinu ya
utoaji tiba ili wananchi wapate huduma stahiki. Ombi la
hospitali ya wilaya nimelipokea na nitafuatilia kujua limefikia hatua gani,”
alisema.
Kuhusu ujenzi
wa barabara za kuunganisha wilaya, Waziri Mkuu alisema Serikali itaanza kufanya
upembuzi na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka Arusha –
Kiteto – Kongwa ili ijengwe kwa kiwango cha lami.
Kuhusu
migogoro ya ardhi iliyotajwa na wananchi kwenye mabango yao, Waziri Mkuu
alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Simanjiro, Eng. Zephania Chaula aende na mbunge
huyo kwenye maeneo yanayolalamikiwa na wananchi ili akabaini chanzo cha
migogoro na aitafutie ufumbuzi.
Kuhusu umeme,
Waziri Mkuu alisema vijiji 18 katika ya 57 vya wilaya vimeshapatiwa umeme na
vilivyoakia vimeshaingizwa kwenye mpango wa serikali wa kuvipatia umeme vijiji
8,000.
Aliwaonya
wakazi wa Mererani wachukue tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI
kwani takwimu zinaonyesha kuwa kasi ya maambukizi katika mji huo iko asilimia
18 kiwango alichosema ni kikubwa kuliko kiwango cha kitaifa.


0 comments:
Post a Comment