Usiku wa Jumapili hii katika ukumbi wa Dolby Theatre, Hollywood nchini Marekani zilifanyika sherehe za utoaji tuzo za 89 za Oscar.
Kubwa zaidi lililoteka ni moja ya mpuyango ambao hujategemewa katika tuzo hizo ambapo baada ya filamu ya La La Land kutangazwa kuwa filamu bora na baada ya waigizaji wa filamu hiyo kuingia jukwaani tayari kutoa hotubazao za ushindi huo mmoja wa watayarishaji wa tuzo hizo aliingia na kutangaza kuwa tuzo hiyo imetolewa kimakosa na filamu iliyoshinda ni Moonlight.
Mbali na hilo mpuyango mwingine ulioibuwa maswali mengi ni baada ya Bahasha aliyopewa Warren Beatty kutangaza kipengele cha Picha bora ya Mwaka (Best Pictures) katika tuzo hizo ilikuwa imeandikwa Muigizaji bora wa Kike aliyeigiza vizuri “Actress in a Leading Role”.

0 comments:
Post a Comment