Good news kwa wadau wote na wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva, bila kuwasahau wazalendo wote wale ambao hupenda vya nyumbani kwanza.
Kituo cha MTV Base kimetoa list ya wasanii 50 kutoka kila kona barani Africa ambao wanataarajiwa kufanya makubwa kwa mwaka huu wa 2017.
Kutoka Bongo Land Tanzania ni vichwa 4 ndivyo ambavyo vimebahatika kukaa kwenye list hiyo, ambavyo ni Billnass hitmaker wa ngoma ya Chafu Pozi, Benpol ambaye anatamba na ngoma yake ya Phone, kutoka WCB Wasafi ni kijana Rayvanny pamoja na mwanadada Ruby.
Ni ishara tosha kwamba muziki wetu sasa hivi unasikilizwa na kutazamwa kila kona, ikiwa ndio jambo kubwa ambalo tulikuwa tukilihitaji miaka yote. Cha msingi ni kuendelea kusapoti muziki mzuri ili tuzidi kufika mbali zaidi.
Unahisi ni msanii gani mwingine kutoka Tanzania alistahili kukaa kwenye list hiyo halafu hajawekwa? Niandikie kwenye uwanja wa comments hapa chini nami nitapita nayo kama kawiz.
0 comments:
Post a Comment