Kama tunavyofahamu, uhusiano wa kimapenzi wa watu wawili utaonekana kuwa serious pale mmoja anapoamua kufunga safari kumtambulisha mpenzi wake kwa wazazi na ndugu wengine.
Mwishoni mwa mwaka jana Rapper AKA aliripotiwa kumpeleka mpenzi wake Bonang Matheba kwa wazazi wa wazazi wake (babu na bibi). Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu vya Rapper huyo vilidai, AKA alimpeleka mpenzi wake huyo jijini Cape Town kusherehekea sikukuu ya Christmas na familia yake.
Sasa sad news nikwamba, Ijumaa hii ya Feb 17, Rapper wa Afrika kusini, AKA ametangaza rasmi kuachana na mpenzi wake Bonang Matheba ambae ni Mtangazaji maarufu nchini humo. AKA alitumia akaunti yake ya Twitter kutoa taarifa ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake.
Yadaiwa kuwa kabla ya dakika 10 kuweka ujumbe huo (hapo juu) alidokeza ukweli kwamba kuna kitu kilikuwa hakipo sawa baina yake na mpenziwe.
Hii si mara ya kwanza kwa wawili hao kuwa hivi, walishawahi kuwa na tifu la hatari, pia walitumia njia hihi ya kutangaza hadharani.
0 comments:
Post a Comment