Wednesday, February 8, 2017

Rita Dominic
Na MWANDISHI WETU |
ZIKIWA zimepita saa chache tangu atupie picha mtandaoni ikimuonesha akiwa na nguo zilizomzidi mwili ‘oversize’, mashabiki wa mkongwe wa filamu kutoka Nollywood, Rita Dominic wameamua ‘kumchana live’ kuwa anaendelea kujizeesha.
Rita Dominic
Hivi karibuni, Rita mwenye miaka 41 anayetikisa kwa filamu kibao ikiwemo Angel of Love na Deadly Love alitupia picha kwenye mitandao ya kijamii ikimuonesha katika muonekano tofauti ambapo kwa upande wa juu alivaa shati kubwa lililoufunika mwili wake pamoja na sketi.
“Umependeza dada ila tatizo kidogo, hayo mavazi yanakuzeesha, huna kioo? Kwa hilo vazi umeniboa.” Ilisomeka moja ya komenti.

0 comments:

Post a Comment