Tuesday, February 28, 2017


Kocha wa mwanariadha Mo Farah, Alberto Salazar amekanusha vikali taarifa za kwamba anarudidha nyuma jitihada za kupiga vita dawa zilizokatazwa michezoni.


Alberto Salazar raia wa Marekani amekuwa chini ya upelelezi maalum kutoka mwkaa 2015 mara baada ya kipindi cha BBC Panorama kkumhusisha na kashfa ya kuwasaidia baadhi ya wanariadha kupata dawa zinazosisimua misuli katika kambi ya wachezaji wa Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti iliyovuja ilieleza kwamba Salazar alimpatia mwanariadha Mo Farah pamoja na wanariadha wengine dawa za kusisimua misuli aina ya L-carnitine.
Licha ya kushukiwa na kujihusisha huko, Alberto amesema anaamini katika mchezo ulio msafi, pamoja na mazoezi ya kutosha na haungi mkono matumizi ya dawa zilizokatazwa michezoni na anaunga mkono juhudi za Wada pamoja na IAAF.
Mwanariadha Mo Farah

Kocha huyo amesema katika kuonyesha namna anavyounga mkono jitihada za WADA amewasiliana na USADA na amekuwa akijitolea kutoa ushirikiano wa kutosha.
Katika michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 iliyofanyika nchini Brazil, Mo Farah alikuwa mwanariadha wa kwanza kutoka nchini Uingereza wa mbio na uwanjani kushinda medali tatu za dhahabu katika mbio za mita 10,000 mjini Rio.

Mo Farah alijikwaa wakati wa mbio hizo, lakini aliinuka na kujikaza vilivyo katika mita 100 za mwisho na kushinda kwa muda wa dakika 27 sekunde 5.

0 comments:

Post a Comment