Tuesday, February 7, 2017

Serikali inatarajia kupiga marufuku utengenezaji na uingizaji wa pombe za bei rahisi maarufu kama ‘Viroba’ Nchini, ndani ya miezi mitatu ijayo.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia kilevi hicho kinavyopunguza nguvu kazi ya Taifa.
Waziri Kigwangalla amesema kuwa baada ya miezi mitatu kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na kuziba mianya yote ya uingizaji wa kilevi hicho ambacho kimekuwa kikitumiwa na vijana wengi, hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko amesema pombe hiyo inasababisha vifo vya vijana wengi nchini ambao ndio tegemeo kubwa na nguvu kazi ya Taifa. “Katika kipindi hiki kifupi cha likizo yangu, nilikuwa jimboni kwangu na tumezika vijana wanne ambao wamefariki kutokana na matumizi ya viroba. Hivyo wananchi wa jimbo langu wameniagiza kuja kulieleza Bunge athari za pombe hiyo ili tuweze kujadili na kuona namna gani ya kuliokoa taifa hasa vijana kutoka katika janga hilo,” alifafanua Matiko.
By: Emmy Mwaipopo

0 comments:

Post a Comment