Friday, February 24, 2017


 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye amewataka Watanzania kuwa wastaarabu na wazalendo kwa kutokuharibu miundumbino ya uwanja wa Taifa katika mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga.

Akiuzungumzia mchezo huo unaotaraji kupigwa siku ya jumamosi Waziri Nnape amesema vyombo vya ulinzi pamoja na usalama vimejipanga vya kutosha ili kudhibiti usalama wakati wa mchezo huo.


Katika hatua nyingine Waziri Nape ameitaka TFF pamoja na bodi ya ligi kuhakikisha inapanga waamuzi bila kutazama maslahi yao binafsi.
Waziri nape amesema ni vema wakateuliwa waamuzi watakaotafsiri vema sharia ili yule atakaefungwa afungwe kwa haki bila uonevu.

0 comments:

Post a Comment