Monday, February 20, 2017



Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), limekamilisha hatua ya kwanza na ya muhimu ya maandalizi ya kuelekea Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika ‘World Cross Country’ zitakazofanyika Kampala Uganda Machi 26, Mwaka huu.


Jumamosi, Februari 18 RT iliendesha Mashindano ya Taifa ya Mbio za Nyika katika Viwanja vya Gofu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na kushirikisha mikoa zaidi ya 11 Tanzania Bara na Visiwani, ambapo wakongwe wengi wa riadha wamekiri kwamba mwamko waliouona juzi haujatokea tangu mwaka 1991 kwenye mashindano yaliyofanyika Arusha eneo la Mushono.

Mwaka huo wa 1991, ndiyo mwaka ambao mtanzania pekee Andrew Sambu alishinda mashindano ya Junior ya Dunia Antwerp Belgium, kwa mfano huo sisi Shirikisho la Riadha Tanzania tuna imani kubwa na timu iliyochaguliwa mwaka huu, tunakwenda Uganda kifua mbele, hatuogopi chochote, mataifa mengine nayo yanafahamu kwamba watanzania wameamua safari hii.

Majina ya wanariadha waliochaguliwa kwenda kusaka medali Uganda na kupeperusha vyema bendera yetu.
Waliochaguliwa kwenye timu ya Taifa kwenda Kampala ni wafuatao:

Wanaume Senior 10KM;
1)      Emmanuel Giniki – Manyara
2)      Basil John – CCP / Kilimanjaro
3)      Gabriel Geay – JKT / Arusha
4)      Fabian Joseph – Arusha
5)      Wilbado Peter – CCP / Kilimanjaro
6)      Josephat Joshua – CCP / Kilimanjaro

Wanawake Senior 10KM;
1)      Magdalena Shauri – JKT / Arusha
2)      Angelina Tsere – JKT / Arusha
3)      Failuna Abdi – Arusha
4)      Sara Ramadhani – Arusha
5)      Jackline Sakilu – JWTZ / Arusha
6)      Siata Kalinga – JWTZ / Arusha

Wanaume Junior 8KM;

1)      Francis Dambel – Manyara
2)      Yohana Elisante – JKT / Arusha
3)      Ramadhani Juma – Arusha
4)      Elisha Wema – Arusha
5)      Anthony Wema – Arusha
6)       Joshua Elisante – Arusha

Wanawake Junior 6KM;
1)      Cecilia Ginoka – JKT / Arusha
2)      Maicelina Issa – JKT / Arusha
3)      Asha Salum – JKT / Arusha
4)      Noela Remy – Manyara
5)      Elizabeth Boniface – Singida
6)      Amina Mgoo – JKT / Arusha

Timu ya Relay Wanaume wawili;
1)      Faraja Damas – JKT / Arusha
2)      Marco Sylvester – Singida
Timu ya Relay Wanawake wawili, itangazwa hivi karibuni kutokana na sababu za kiufundi.

Makocha wa timu ya taifa;
Kamati ya Ufundi ya RT, imewapendekeza wafuatao kuwa makocha wa timu hii ya Taifa.

1)      Naasi Gwagwe Dengwe – CCP
2)      Thomas John Tlanka– Arusha
3)      Francis Nade – Manyara
4)      Zakaria Barie – Arusha
5)      Lwiza John - Mbeya

0 comments:

Post a Comment