Friday, February 10, 2017



Wachezaji wa mchezo wa bao kutoka katika klabu ya Sisi kwa Sisi yenye maskani yake Manzese jijini Dar es Salaam wapo katika mazoezi makali wakijiandaa kwaajili ya mchezo wa mardiano dhidi ya klabu ya Kizota ya Mburahati.


Katika mahojiano na Blogu ya Wananchi mmoja wa wachezaji wa Sisi kwa Sisi Thomson Kauchungu amesema timu yake ilipoteza katika mchezo wa awali kwa kukubali kichapo toka Kizota hivyo sasa wanataka kufuta uteja.

Nae mwenyekiti wa sisi kwa sisi Mzee Mohamed Mkumba amewataka wadau na mashabiki wa kizota wajiandae kupokea kipigo kikali kwani wachezaji wa klabu yake wamejipanga vya kutosha.
Mkumba amesema wachezaji wa sisi kwa sisi wamekuwa wakifanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha viwango vyao.

Katika hatua nyungine Rais wa Shirikisho la mchezo wa bao nchini Shibata Monday Likwepa amesema mchezo huo utakuwa ni wa kusisimua kutokana na upinzani uliopo pamoja na viwango vya wachezaji toka katika vilabu vyote viwili.

0 comments:

Post a Comment