Baada ya picha mbali mbali za J Lo na Drake kusambaa kila kona ya mitandao ya kijamii huku kukiwa na taarifa kwamba wawili hao wanatoka kimapenzi, bad newz ni kwamba wawili hao sasa hawapo tena pamoja.
Kupitia mtandao wa The Jasmine Brand umeripoti kwamba kapo hiyo imevunjika na ukaribu wao sasa sio kama uliokuwa mwanzo, licha ya mtandao huo kuripoti taarifa hizo, watu wakaribu wa Drake nao waliamua kufunguka na kusema kwamba “wawili hao wamejipatia muda kidogo wakuwa mbali kutokana na ratiba za kazi zao kuwabana kuwa pamoja”.
Kama utakumbuka mwezi uliopita Drake na J.Lo waliwahi kuonekana wakipeana kisses huko mjini L.A, kama unavyojua wawili hao wote wapo kwenye Tour zao ambazo ndizo zinawafanya kuwa bize ya kuwa pamoja.
0 comments:
Post a Comment