Thursday, February 2, 2017

Afisa Mahusiono Eric Mkomoye (mwenye shati jeupe ) na meneja wa mitandao Kelvin Boniface wakipokea cheti cha ushindi kwa TECNO MOBILE, Kampeni bora ya mwaka katika mitandao ya Kijamii 2016 
Kampuni inayoongoza kwa mauzo ya simu nchini Tanzania, TECNO MOBILE imefanikiwa kushinda tuzo za Tanzania leadership Awards zilizofanyika mwishoni mwa wiki Jijini Dar es salaam. 
Katika mchakato wa tuzo hizo zilizoandaliwa na Purple cow media Tecno iliingia katika tatu bora ikiwa inashindana na kampuni mbili kubwa nchini Tanzania, kampuni ya mawasiliano ya simu TIGO na kampuni ya vinywaji TBL , zote zikiwa katika kitengo cha kampeni bora MITANDAO YA Kijamii ya mwaka katika mitandao ya kijamii. 
Tecno waliingia katika kinyang’anyiro kupitia kampeni yao ya simu maarufu ya TECNO CAMON C9, katika kampeni iliyoshika hisia za watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii kutokana na kuwapa nafasi watumiaji wa simu kupiga picha kutokana na maelekezo yaliyokua yanatolewa na account za mitandao ya kijamii za kampuni, washiriki washindi walipewa zawadi za aina mbalimbali zikiwemo simu za TECNO CAMON C9.
Tecno imekua kampuni ya kwanza ya simu kushinda katika kategori hiyo ya kampeni bora ya mwaka ya mitandao ya kijamii kutokana na uwezo wake mkubwa uliojidhihirisha kwa kuwapa nafasi kubwa watumiaji wa mitandao na wateja wake kufikisha matzo yao na kusaidiwa lakini pia wateja kuongea na watu mbalimballi maarufu kama Salma Jabir, Hamisa Mobeto pamoja na Idriss Sultani huku zawadi kemkem zikitolewa kwenda kwa watumiaji wa mitandao waliofwata TECNO mobile katika mitandao.Jamii ya Kitanzania itaendelea kufaidika na mitandao ya kijamii kupitia kampuni kubwa ya Tecno Mobile wakifanya matukio mbalimbali ikiwemo kampeni mpya iliyopata umaarufu ya KAMA MBELE washindi wakipata nafasi ya kwenda kushudia mchezo wa mpira wa miguu katika jiji la Manchester wakiwa na mchekeshaji Idris Sultan, pamoja na Kampeni UPENDO inayowataka watumiaji kuweka picha au video mitandao wakisema upendo kwao ni nini na video/picha bora itampa nafasi mshiriki kuchaguliwa kwenda kusheherekea siku ya wapendao katika hotel kubwa Nchini. 

0 comments:

Post a Comment