Klabu ya Azam FC, inataraji
kushuka dimbani siku ya kesho kuwakabili maafande wa Ruvu Shooting, katika
mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani Pwani.
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd
Nassor Cheche, amesema kuwa kikosi chake kinakwenda Mabatini kuendeleza wimbi
lao la ushindi kwa kuichapa Ruvu Shooting.
Cheche amesema wanandinga wa Azam
FC wapo katika morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na
mazoezi makali wanayopewa chini ya benchi la ufundi linaloongozwa na Mromania,
Aristica Cioaba, pamoja na wasaidizi Msaidizi wake, Idd Cheche na Kocha Makipa,
Idd Abubakar.
0 comments:
Post a Comment