Ben Pol, Barakah The Prince na Jux, Jumamosi ya February 18 waliungana kufanya show pamoja yenye theme ya Valentine’s. Show hiyo ambayo iliipewa jina ‘Love, Melodies & Lights’ LML. Watatu hao, Walikuwa katika jukwaa moja lenya sura ya upendo, muziki mzuri wa kugusa nafsi, na yote ilikuwa katika mwanga fulani unaoakisi hisia nzuri.
Good news nikwamba watatu hao, Ben Pol, Baraka the Prince na Juma Jux (Jux) wamechanga Sh 800,000 kwa ajili ya kumsaidia msanii mwenzao, Jet Man, anayehitaji fedha kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa maradhi yanayomsumbua yanayomsababishia asiweze kutembea.
Jux, Ben Pol & Barakah The Prince
Ben Pol alifafanua kwamba, baada ya onyesho lao la Love, Melody and Lights, katika fedha walizoingiza walitoa Sh 500,000 na pia wasanii hao walinunua biti iliyotengenezwa na Jet Man kwa kila mmoja kutoa Sh 100,000 kila mmoja, zikawa Sh 800,000 wakampelekea msanii huyo ili zimsaidie.
“Katika fedha tulizoingiza tumetoa Sh 500,000 na pia tumeongeza kila mmoja Sh 100,000, imefika Sh 800,000 tumempa rafiki yetu na msanii mwenzetu kwa mapenzi yetu ili zimsaidie katika baadhi ya mahitaji yake,’’ Ben Pol aliliambia gazeti la mtanzania.
Ben Pol aliongeza kwamba, licha ya kusaidia kiasi hicho pia wasanii hao wakishirikiana na mchekeshaji Mc Pilipili wameandaa tamasha mkoani Dodoma (lilifanyika siku ya jana) ambalo pia watatenga kiasi cha fedha kwa ajili ya kumchangia msanii huyo mwenye uhitaji mkubwa wa fedha kwa ajili ya kufanyiwa tiba ya matatizo yanayomsumbua.
Kuhusu Jet Man
Jetman ni producer na msanii wa dancehall anayeishi Mwanza, aliyewahi kufanya vizuri miaka ya nyuma na vibao mbalimbali. Na sasa anahitaji msaada kutoka kwa wadau ili aweze kurejea kwenye hali yake ya kawaida.
0 comments:
Post a Comment