Posted by Williammalecela.com on Thursday, February 16, 2017
 |
Serikali kupitia Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) imeufungia wimbo
wa Nikki Mbishi wa "I AM SORRY JK" kwa madai kuwa maudhui ya wimbo huo
ni kinyume na maadili.
Kufuatia katazo hilo, serikali imepiga marufuku
wimbo huo kuchezwa katika chombo chochote cha habari na katika maeneo ya
umma. Pia mtu (binafsi) atakayekamatwa anausikiliza wimbo huo
(nyumbani, kwenye gari etc) atachukuliwa hatua za kisheria.
Uamuzi huo umekuja saa chache baada ya rapper huyo kuitwa na Baraza la Sanaa
la Taifa, BASATA Jumatano hii kujielezea kuhusiana na wimbo huo.
Kupitia Instagram, Nikki amewaonya watu kuusambaza wimbo huo kwakuwa
mkono wa sheria utawaangukia.
“Naomba niombe radhi kwa vyombo vyote vya habari kuwa sitoweza kuwapa
ushirikiano wowote kuhusu wimbo wangu wa “I’M SORRY JK” uliositishwa na
hii ni kwa usalama wao na wangu pia,” ameandika Nikki kwenye Instagram.
|
0 comments:
Post a Comment