Afrika
kusini imeenguliwa katika uenyeji wa wa michezo ya jumuiya ya madola yaani Commonwealth
iliyokuwa imepangwa kufanyika katika jiji la Durban 2022.
Akitaja
sababu ya Jiji la Durban kutohodhi tena michezo hiyo, Mkurugenzi mkuu wa
michezo hiyo David
Grevemberg, amesema jiji hilo limeshindwa kufikia vigezo na masharti waliyokuwa
wamepewa.
Mapema mwezi uliopita waziri wa
Michezo wa Afrika Kusini Fikile Mbalula alisema michuano hiyo isingeweza
kufanyika nchini Afrika Kusini kutokana na matatizo ya kiuchumi.
Waziri Fikile alisema serikali ya
Afrika Kusini ilijitahidi kuhakikisha maandalizi hayo yanakamilika kwa wakati
lakini Serikali haina fedha hivyo hawawezi kuandaa tena michezo hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri huyo
amesema kutokana na ukata huo wameona ni vema wkaiacha serikali itatue kwanza
changamoto zinazoikabili ikiwa ni pamoja
na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wa Afrika kusini.
Durban ilipewa nafasi ya kuandaa
michezo hiyo mwezi September 2015 na kama michezo hiyo ingefanyika ingekuwa ni
mara ya kwanza kwa michezo hiyo iliyoanza mwka 1930 kufanyika barani Afrika.
Sasa miji ya Liverpool na Birmingham
ndio ambayo imeonyesha nia ya kutaka kuhodhi michezo hiyo inayotaraji kufanyika
2022.
Msemaji wa jii la Liverpool ndie
ambae amethibitisha kwamba jiji hilo linaweza kutumika kama mweyeji wa michuano
hiyo.
Kwa upande wa jiji la Birmingham maandalizi
ya michezo ya jumuiya ya madola ya mwaka 2026 yameshaanza hivyo Diwani wa jiji
hilo Ian Ward, amesema wanaweza kuwa wenyeji wa michezo ya mwka 2022 pia.
Ian amesema tayari miundombinu ya
miichezo mbalimbali imeshaanza kutengenezwa hivyo jiji hilo halitakuwa na kazi
kubwa katika maandalizi ya 2022.
Atakaepata fursa ya kuhodhi
michuano hiyo atatangazwa mwishoni mwa mwaka huu.
Michezo ya jumuiya ya madola
hufanyika kila baada ya miaka mine ikishirikisha wanamichezo wa michezo
mbalimbali toka katika mataifa 50 ambayo yameshawahi kuwa makoloni ya Uingereza.
0 comments:
Post a Comment