Wednesday, March 29, 2017



Kuelekea katika mchezo wa April Mosi utakaowakutanisha mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara kalabu ya ya Yanga dhidi ya klabu ya Azam FC, Uongozi wa Azam umeanza kujinadi kwa kusema kwambaa klabu hiyo itabuka kidedea katika mchezo huo.


Akizungumza na Mbungi ya Afrika Swahili TV Afisa Habari wa Azam FC Jaffry Iddy Maganga amesema licha ya kwamba Azam imeachwa kwa alama 11 klabu hiyo itapambana kufa na kupona ili kuhakikisha inakusanya alama tatu katika michezo yote iliyosalia katika ligi kuu ya Vodacom katika msimu huu wa 2016/2017.
Jaffary amesema wanandinga wote wa Azam FC wameingia kambini leo Jumatano.

Katika hatua nyingine Jaffa amewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo wanaodhani kwamba wanandinga wa Azam waliokuwa wamejumuishwa katika timu ya taifa watakosa utimamu kutokana na kujumuishwa katika chezo dhidi ya Botswana pamoja na mchezo dhidi ya Burundi.

Wachezaji wa Azam Fc waliokuwa wamejumuishwa katika timu ya taifa ni Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Gadiel Michael, Himid Mao, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo.

Wakati huohuo japha amesema uongozi wa klabu ya Azam FC umeridhishwa na kiwango ambacho mwanandinga farid Musa amekionyesha katika majukumu yake ya Timu ya taifa.

Farid anakipiga kwa mkopo katika klabu Deportivo Tenerife inayoshiriki katika Ligi Daraja la Pili Hispania (Segunda)

0 comments:

Post a Comment