Basi la
RUKSA CLASSIC lenye namba za usajiri T636AWC likitoka jijini Mwanza
kwenda mkoani Kigoma limegongana uso kwa uso na gari dogo lenye namba za
usajiri T 210 DJJ katika kijiji cha Nhelegani mkabala na chuo cha
Ushirika Moshi kambi ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.
Chanzo
cha ajali hiyo iliyotokea majira ya nne asubuhi inaelezwa kuwa ni
uzembe wa dereva wa gari ndogo ambaye hakuwa na utulivu barabarani na
kujikuta yupo upande usio sahihi na kusababisha ajali.
Hata
hivyo hakuna mtu aliyepoteza maisha ingawa dereva wa gari dogo na abiria
wake mmoja, wameumia na kukimbizwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa
Shinyanga.Mwandishi mkuu wa MASENGWA BLOG Isaac Luhende alifika eneo la tukio mapema kabisa na ametuletea picha za tukio hilo
Basi likiwa limegongana uso kwa uso na gari dogo
Basi la RUKSA CLASSIC
Gari dogo likiwa limefunikwa
Basi hilo
Mbele ya basi
Watu wakisaidia kuichomoa gari hiyo
Gari dogo likiwa limeharibika
Watu wakishuhudia tukio hilo
Nyuma ya gari dogo
























0 comments:
Post a Comment