Watu 26 wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kutokea mlipuko wa bomu wakiwa katika sherehe ya harusi (wedding party) karibu na mji wa Tikrit, Iraq.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo alhamisi ya Machi, 9 katika kijiji cha Hajjaj kilichopo kilomita 20 kutoka mji Tikrit limehusishwa na vikundi vya kigaidi.
Mpaka sasa hakuna kikundi cha kigaidi ambacho kimejitangaza kuhusu na shambulio hilo ijapokuwa kikundi cha ISIL kinahusishwa kufanya shambulio kwani awali kijiji hicho kilikuwa chini ya ISIL kabla ya Aprili, 2015 kukombolewa na majeshi ya serikali.
Polisi wameuambia mtandao wa Reuters kuwa katika tukio hilo kulitokea milipuko miwili iliyolipuliwa katika sherehe hiyo na wahusika wa tukio walipanga kulipua mabomu mengine katika kituo cha Polisi.
0 comments:
Post a Comment