Bondia Anthony Crolla amesema anaamini ubinafsi na moyo wa kujiona kwamba yeye ni bora ndio utakaofanya pambano lake la siku ya jumamosi katika jiji la Manchestter liwe la kuvutia sana.
Anthony atashuka ulingoni siku ya
jumamosi kuzichala dhidi ya bondia Jorge Linares ambae ni bingwa wa WBA.
Hii itakuwa ni mara yake yakwanza
kushuka ulingoni ndani ya miezi sita toka alipozichapa dhidi ya bondia Jorge
Linares katika ukumbi wa Manchester Arena.
Akizungumzia maandalizi yake
kuelekea katika pambano hilo, Anthony amesema kasi yake imeongezeka na amekuwa
na ufanisi wa hali ya juu, na amekuwa akifanya mazoezi mazoezi akiwa mafichoni.
Kocha wa Anthony Joe Gallagher ndio
ambae amemwambia bondia wake aw mbinafsi na mwenye hasira ili aweze kupata
ushindi katika pambano hilo.
Pambano hilo linatazamiwa kuwa
zuri na lenye kuvutia kwani mpinzani wa
Anthony anasifika kwa kuwa na makonde mazito akitumia mikono yake yote miwili.
Kutokana na ubora wa mpinzani
wkae Anthony amesema anafahamu pambano huwa gumu pale bondia mmoja anapokutana
na bondia mwingine ambae ni mzuri kwa kiwango lakini kwake ni lazima aufanye
usiku wa pambano hilo katika jiji la Manchester uwe usiku mzuri kwake.
0 comments:
Post a Comment