Meneja wa klabu ya
Manchester City Pep Guardiola amesema ni vigumu sana kuizuia klabu ya Chelsea
isibebe taji l;a ligi kuu soka nchini Uingereza msimu huu.
Pep Guardiola ameyasema
hayo mara baada ya kukamilika kwa mchezo ulioikutanisha klabu yake dhidi ya Sunderland
na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Kwa sasa klabu ya Chelsea inaongoza katika msimamo
wa ligi kuu soka nchini Uingereza ikiwa na jumla ya alama 63 na mchezo mmoja
mkononi dhidi ya West ham United.
Klabu inayoifata Chelsea kwa karibu ni klabu ya Tottenham
ikiwa nyuma kwa alama 7 na sasa itakutana na Stoke siku ya jumatano.
Guardiola amesema tofauti ya alama ni kubwa sna na Chelsea nayo imekuwa
ikifanya kazi kubwa kila inaposhuka dimbani kwani haizuiliki hata kidogo.
0 comments:
Post a Comment