
Miezi michache iliyopita tulizipata habari za mkali wa muziki aliye chini ya lebo ya Endles Fame ya mwanadada Wema Sepetu, Mirror kupata ajali mbaya ya gari na kuripotiwa kuvunjika mguu.
Ilisikika kwamba gari ambayo ilihusika kwenye ajali ya Mirror ilikuwa ni mali ya mwanadada Wema Sepetu, Shilawadu wakatupenyezea kwamba kitendo hicho kilimkera sana Wema Sepetu hadi kufikia hatua ya kumtelekeza msanii wake huyo kutokana na kipindi alopochukua gari hiyo na kutoka nayo hakuomba.
Soudy Brown ameamua kulivalia njuga jambo hilo na kumtafuta Mirror na kupiga nae story ili aweze kufunguka ukweli kuhusu kutelekezwa na meneja wake Wema Sepetu wakati huo wa ugonjwa.
Mazungumzo ya wawili hao nimekuwekea kwenye video hii hapa chini, unachotakiwa kufanya ni kubonyeza play kwenye video hii hapa chini na kusikiliza mwanzo hadi mwisho.
0 comments:
Post a Comment