Wednesday, March 22, 2017


Mcheza tennis Petra Kvitova has regaiamepata nafuu na sasa ameanza taratibu kuutumia mkono wake kushika raketi na kuanza kucheza tennis katika mazoezi madogomadogo toka aliposhambuliwa kwa kuchomwa kisu mwezi December mwaka jana.

Kvitova, 27, alivamiwa na mtu mmoja aliekuwa na kisu na kasha akamshambulia akiwa Prostejov katika jamhuri ya watu wa Czech.

Madaktari wamesema kwamba mchezaji huyo ambae ni bingwa wa michuano ya Wimbledon ya mwaka 2011 na mwaka 2014 Wimbledon anaweza akawa fiti ndani ya miezi sita.

Akizungumza na wanahabari msemaji wake amesema Petra anaendelea vizuri na anaamini kwamba atarejea tena viwanjani kwa wkati.


Amesema kwa sasa tayari Petra ameanza vema kuutumia mkono wake katika shughuli zake za kila siku lakii hawezi kusema ni lini hasa atarejea tena katika mchezo wa tennis.

0 comments:

Post a Comment