Wednesday, March 22, 2017


Uongozi wa klabu ya Azam umeapa kutokuchukua hatua zozote ikiwemo ya kuandika barua kwenda katika shirikisho la mchezo wa soka barani Africa CAF kuhusu vurugu walizofanyiwa nchini Swaziland walipokwenda kukipiga katika mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya klabu ya Mbabane Swalows kwani msimamizi wa mchezo huo alishuhudia vurugu zote ambazo Azam FC walifanyiwa.


Akizungumza na Mbungi ya Afrika Swahili TV Afis habari wa Azam FC JAphary Iddy Maganga amesema kilichowapeleka Swaziland ilikuwa ni kutafuta matokeo ya uwanjani na kkukiri kwamba wapinzani wao walikuwa wazuri kuwazidi.

Katika mchezo huo Azam FC walizuiwa kuingia na basi lao uwanjani, lakini pia wakalazimika kubadilishia nguo katika basi hilo kwani katika chumba chao cha kubadilishia nguo kulikuwa na hewa nzito sana, hali iliyoashiria kwamba kuna hewa Fulani ambayo ilipulizwa katika chumba hicho ili kuwachosha wanandinga wa Azam.

Japha Iddy amekiri kwamba changamoto ya kukabiliwa na majeruhi wengi imechangia pia kupoteza katika mchezo huo.

Wakati huo huo Japha amesema kikosi cha Azam kinataraji kuanza mazoezi yake siku ya Alhamisi tayari kwaajili ya mchezo dhidi ya klabu ya Yanga utakaopigwa April mosi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Klabu ya Azam kwa sasa haipo katika mbio za kuwania ubingwa wa EPL lakini Japha ameahidi kwamba mpango wa kocha wa klabu hiyo ni kuhakikisha anapata matokeo katika michezo yote iliyosalia pamoja na kutwaa taji la Kombe la Shirikisho na hatimae iweze kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya kimataifa msimu ujao.

0 comments:

Post a Comment