Wednesday, March 1, 2017


Vilabu vya soka nchini China vimetumia jumla ya paundi 331 milioni kwa kuzinasa saini za wanandinga mbalimbali wakiwemo wale waliokipiga katika ligi kuu soka nchini Uingereza hadi kufungwa kwa dirisha la usajili wakati wa majira ya joto.

Dirisha la usajili nchini China limefungwa usiku wa February 28 na kuzishuhudia klabu 16 zinazoshiriki katika Chinese Super League zikigonga hodi katika vilabu mbali mbali nchini Uingereza.

Mwanandinga wa zamani wa klabu ya Chelsea, Oscar amejiunga na Shanghai SIPG kwa dau la £60 milioni huku klabu ya Shanghai Shenhua ikimnasa Carlos Tevez  kwa dau la £40 .

Kwa mujibu wa sharia zilizopo nchini China, wachezaji watatu tu wa kigeni ndio watakaoruhusiwa kuanza katika mchezo mmoja.

0 comments:

Post a Comment