Timu ya Uingereza katika mchezo wa Cricket itakutana
na India katika mashindano ya Kombe la dunia katika mchezo huo ICC kwa wanawake
huko Uingereza pamoja na Wales.
Mchezo
wa ufunguzi kwa Uingereza utakuwa June 24 huku mabingwa watetezi wa taji hilo
timu ya Australia wakikipiga dhidi ya West Indies huko Taunton June 26.
Uingereza
inashika nafasi ya pili kwa ubora duniani na mchezo wao mgumu utakuwa ni mchezo
wa July 9 dhidi ya Australia in Bristol on 9 July.
Timu
nane zinazoshiriki katika mashindano hayo zitakutana kwa nyakati tofauti
tofauti na baadae timu nne za juu kuingia katika hatua ya nusu fainali na
baadae fainali. Itakayopigwa tarehe 23 July
Mataifa
yote yatakaoingia katika fainali hizo ni pamoja na Australia, Uingereza, New
Zealand, pamoja na West Indies.
Mataifa
mengine ni pamoja na Afrika Kusini, India, Sri Lanka pamoja na Pakistan.
Mtendaji
mkuu wa ICC David Richardson, amesema hadi sasa tayari zaidi ya tiketi 9,000 za
mchezo wa fainali zimeshanunuliwa.
David
amesema wanatarji kwamba michuano hiyo itakuwa mizuri na yenye msisimko wa hali
ya juu kwani wachezaji wamejipanga kutafuta ubingwa hivyo upinzani utakuwa wa
hali ya juu.
0 comments:
Post a Comment