Katika mchezo huo Konta, anaeshikilia nafasi ya 10 kwa ubora duniani
alishinda kwa seti s 6-4 6-0 ndani ya dakika 63.
Kutokana na ushindi huo, sasa Konta atakutana na Lara Arruabarrena ambae
alipata ushindi wa seti 7-5 7-5.
Kufanikiwa kwa Konta, 25, kufika katika hatua ya 16 bora ni mafanikio
makubwa kwani katika michuano mikubwa kwa mwaka huu amekuwa akipata wakati
mgumu sana toka alipotolewa katika hatua ya robo fainali katika michuano ya
wazi ya Australia mwezi januari mwaka huu.
Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo, Konta amesema amefurahishwa
sana na matokeo ambayo ameyapata kwani ilimlazimu kupigana kufa na kupona ili
kupata matokeo hayo.
Katika mchezo mwingine mchezaji nambari moja kwa ubora duniani Angelique
Kerber amefanikiwa kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Shelby Rogers kwa
kumtandika kwa seti 6-4 7-5.
Sasa Angelique Kerber atakutana na Mjapan Risa Ozaki, ambae amepata
ushindi mbele ya Julia Goerges kw akumfunga kwa seti 7-6 (7-5) 6-3.
Kwa upande wa wanaume mchezaji mmoja mmoja Kei Nishikori toka Japan
amepata ushindi wa seti 7-6 (7-2) 6-7 (5-7) 6-1 dhidi ya Mhispania Fernando
Verdasco anaeshikilia nafasi ya 25 kwa ubora duniani.
Mchezaji Milos Raonic toka Canada yeye amelazimika
kujitoa katika michuano hiyo kutokana na kusumbuliwa na msuli wa mkono. Milos
alitakiwa kucheza dhidi ya Jared Donaldson.
Kwa upande wa wachezaji wawili wanaume, Jamie Murray pamoja na Bruno
Soares waliwashinda Paolo Lorenzi na Joao Sousa kwa seti 6-0 6-3 katika
mzunguko wa pili.
0 comments:
Post a Comment