Thursday, March 16, 2017


Watanzania wameombwa kujitoa kwa hali na mali ili kuiwezesha timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 Serengeti Boys iweze kufanya vema katika fainali za AFCON kwa vijana zitakazofanyika Gabon Mwezi May.



Akizungumza na wanahabari Mwanahabari nguli nchini ambae pia ni Mwenyekiti wa KAMATI YA HAMASA SERENGETI BOYS Charles Hilary amesema mpango uliopo ni kuhakikisha Serengeti inamaliza katika nafasi mbili za juu katika kundi Kundi B ambalo linajumuisha timu za Angola, Mali na Niger ili ipate nafasi ya kushiriki katika kombe la dunia kwa vijana, hivyo ni vema watanzania wakajitoa kwa hali na mali.

Katika mkutano huo ambao ndio mkutano wa kwanza wa wajumbe wa kamati hiyo na wanahabari toka ilivyoteuliwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye, Charles ameweka wazi mipango mbalimbali ambayo wamejiwekea ili kuhakikisha fedha inapatikana kwaajili ya kuwezesha mambo mbalimbali yanayohitaji fedha.

Mipango hiyo ni pamoja na kuangalia uwezekano wa kuchangisha fedha toka katika Halmashauri mbali mbali zilizopo nchini, makampuni mbali mbali, pamoja na michango toka kwa wadau na wapenzi wa soka.

Nae Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano amesema mfumo kwaajili ya kuwawezesha Watanzania kuichangia fedha Serengeti boys umeshakamilika na watumiaji wa mitandao yote wanaweza kutuma fedha kwenda nambari 223344.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo ameipongeza kamati hiyo kwa yale ambayo wameyafanya hadi sasa licha ya kuwa wamepewa majukumu hayo ndani ya kipindi kifupi.
 
Yusuph SIngo amewtaka pia watanzania kuchanga Fedha bila wasiwasi kwani kamati hiyo ni kamati inayowahusisha watu waadilifu.


Katika hatua nyingine mtangazaji nguli wa habari za michezo nchini Maulid Kitenge amesema tayari mdundo maalumu umeshaandaliwa ili kuwawezesha wasanii mbalimbali wa muziki wakiongozwa na Msanii Diamond Plutnumz na Alikiba ili uweze kutumika kuwahamasisha Wapenzi na wadau wa soka nchini waweze kujitoa kwaajili ya Serengeti Boys.

0 comments:

Post a Comment