Mabondia nchini Tanzania wameaswa kuwa
na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kujua kama kuna matatizo
yanayowakabili ili waweze kuepukana na kadhia mbalimbali ikiwemo kupoteza
maisha wanapopanda ulingoni.
Katika mahojiano maalum na Blogu ya
jamii Rais wa Shirikisho la Ngumi Afrika Mashariki na Kati Yasin Abdala Amesema
ni vema mabondia wakawa na utaratibu huo na kuachana na tabia ya kupima afya
zao pale tu wanapokuwa wakitaka kuzipiga katika michezo Fulani.
Yasin amesema toka katika mataifa mbali
mbali wamepoteza maisha kutokana na kukabiliwa na matatizo mbalimbali ya kiafya
wakati walipokuwa wakizichapa ulingoni.
Akitolea mfano matukio yaliyosababisha
vifo vya mabondia kwa hapa Tanzania, Yasin amesema miongoni mwa mabondia
waliopoteza maisha wakiwa ulingoni ni Rajabu
mandela ambae alifikwa na mauti wakati akizichapa na Musa Chipota, wengine ni
Anthony Ndaki ambae aliwahi kuzichapa dhidi ya Charles Kibondo Mawe kutoka
Zambia na kufikwa na mauti akiwa ulingoni kutokana na makonde mazito ambayo
alipokea toka kwa mzambia huyo.
“Matukio haya sio kwamba yanapangwa,
hutokea kwasababu mabondia wanakuwa wamejiandaa kwa sababu kila mmoja anakuwa
anataka ushindi” amesema Yasin.
Yasin amesema kwa upande wa bondia
ambaye humpiga mpinzani wake hadi kufa, bondia huyo hujiandikishia rekodi
nzuri, lakini matatizo yatamfika kama mpinzani wake alikuwa hajafanyiwa vipimo
vya afya ili kubaini kama kweli anaweza kuendelea na mchezo huo.
Wakati huo huo yasin amewataka Mabondi
wa tanzia waishi kwa malengo ili waweze kuzifikia ndoto zao.
Yasin amesema mabondia wengi nchini
wanapoanza kupata fedha hujiingiza katika starehe, hivyo kujikuta wakitumia
fedha nyingi katika mambo yasiyo ya msingi badala ya kutumia fedha hizo kufikia
ndoto walizojiwekea.

0 comments:
Post a Comment