Saturday, March 11, 2017

Juhudi na kujituma ndio vitu ambavyo vinazidi kumzalishia matunda Mtanzania Mbwana Samataa kila kukicha na kuendelea kuifanya Tanzania kujivunia kupitia yeye.

Ni makubwa ambayo amekuwa akiyafanya Mtanzania huyo katika club ambayo anaichezea ya KRC Genk ya nchini Ubelgiji na round hii makubwa hayo yameendelea mpaka kwenye moja kati ya michuano mikubwa sana barani Ulaya, Europa League.
Baada ya kumalizika kwa michezo ya Alhamis iliyopita katika ligi hiyo, jana Ijumaa kilitangazwa kikosi bora cha wiki cha Ligi hiyo na Good News ni kwamba jina la Mtanzania Mbwana Samatta lilikuwemo katika kikosi hicho.
Sio kitu kidogo kwa jina la Mbwana Samatta kuwemo katika kikosi hicho kwasababu kuna majina makubwa duniani kama Zlatan Ibrahimovic wa Manchester United na wengine kibao ambao nao pia wanashiriki katika michuani hiyo lakini hawakubahatika kuwemo katika kikosi hicho.
Hiyo inatoa maana tosha kabisa kuwa uwezo wa Mbwana Samatta ni wa kimataifa na unatosha kabisa kukisanua katika club yoyote ile kubwa duniani.

0 comments:

Post a Comment