Watanzania wameombwa kujitoa kwa hali
na mali ili kuiwezesha timu ya wachezaji wenye ulemavu katika mchezo wa tennis
ili waweze kufanya vema katika michuano ya kombe la Dunia katika mchezo wa
Tennis BNP Paribas World Cup itakayofanyika nchini Itala kuanzia Mei mosi hadi
Mei saba.
Akizungumza na Mbungi ya Afrika Swahili
TV Kocha wa Wachezaji wenye ulemavu Riziki Salum amesema timu hiyo inakabiliwa
na ukata wa fedha hali ambayo imepelekea timu hiyo kushindwa kuweka kambi nje
ya nchi.
Timu niyo inaendelea na mazoezi katika
viwanja vya Gymkana jijini dar es Salaam kwa kufanya mazoezi asubuhi na jioni
kutokana na ratiba za wachezaji kubana.
Riziki amesema tayari jitihada
mbalimbali zimeshaanza kufanyika kwa kushirikiana na chama cha mchezo wa tennis
TTA ili kuhakikisha zinapatikana fedha pamoja na vifaa mbali mbali kwaajili ya
safari ya kuelekea nchini Italia.
Kwa upande wa wachezaji wanaokwenda
nchini Italia John Albert Churu amesema amejitoa kufanya mazoezi katika jua na
mvua lengo lake likiwa ni kuhakikisha Tanzania inafanya vema katika mchezo huo.
Katika hatua nyingine John amewataka
watu wenye ulemavu waachane na tabia ya kuomba mitaani, badala yake wajihusishe
na michezo mbalimbali kwani itawawezesha kutoka kimaisha.
Timu ya Tanzania kwa wanaume ndio timu
pekee kutoka katika bara la Afrika ndio timu pekee inayokwenda kushiriki katika
michuano ya BNP Paribas World Cup.



0 comments:
Post a Comment