Bingwa mtetezi wa michuano ya wazi ya BNP Novak
Djokovic ameanza vema kampeni yake ya kutetea ubingwa wake mara baada ya
kuibuka na ushindi katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Kyle Edmund.
Katika mchezo huo Djokovic alifanikiwa kupata
ushindi wa seti 6-4 7-6 (7-5).
Djokovic alifanikiwa kupata ushindi katika seti ya
kwanza dhidi ya Briton (22) ndani ya dakika 42, lakini katika seti ya pili
alikumbana na upinzani mkali sana kwani Edmund alifanikiwa kupata matokeo
katika michezo mitatu ya mwanzo lakini baadae Djokovic alipambana na
kusawazisha matokeo hayo na kupelekea mchezo huo kuingia katika tie-break.
Mara baada ya kupata matokeo hayo, sasa Djokovic atakutana
na Juan Martin del Potro katika raundi ya tatu mara baada ya Muargentina huyo
kupata ushindi katika mchezo dhidi ya Federico Delbonis. Del potro amepata
ushindi wa seti 7-6 (7/5) 6-3.
Katika hatua nyingine Roger Federer amefanikiwa
kutinga katika hatua ya tatu ya michuano hiyo ni mara baada ya kupata ushindi
wa seti 6-2 6-1 tdhidi ya Mfaransa Stephane Robert.
Federer, alifanikiwa kupata ushindi wa asilimia 79 katika
mipira aliyoanzisha na hivyo kufanikiwa kushinda ndani ya dakika 52.
Mara baada ya kuvuka katika hatua hiyo, sasa
Federer atakutana na Mcheza tennis Steve Johnson. Steve anakutana na Federer
kufuatia ushindi wa seti 6-4 3-6 7-6 (7-4) dhidi ya Kevin Anderson toka Afrika
Kusini.
Licha ya matokeo ambayo ameyapata, Federer mwanzo wa
mchezo wake huo ulikuwa mgumu sana kwake kwani hii ni mara yake ya kwanza
kukipiga dhidi ya Steve Johnson.
Nguli mwingine wa mchezo huo Rafael Nadal nae
amejikatia tiketi ya kusonga katika mzunguko wa tatu mara baada ya kumshinda
Guido Pella na sasa atakutana na Mhispania mwenzake Fernando Verdasco.
Katika michezo yao ya awali Nadal alipata ushindi
wa seti 6-3 6-2 huku Verdasco akipata ushindi wa seti 7-6 (7/5) 6-1 dhidi ya
Mfaransa Pierre-Hugues Herbert.
Kwa upande wa
wanawake Mcheza tenis nambari moja kwa ubora nchini Uingereza Johanna Kontaametupwa
nje ya michuano ya wazi ya BNP Paribas mara baada ya kupoteza kwa seti 6-3 3-6
6-7 (1-7) katika mchezo dhidi ya Caroline Garcia.
0 comments:
Post a Comment