Thursday, March 30, 2017


Mchezaji nambari moja kwa ubora nchini uingereza Johanna Konta amefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali kunako michuano ya wazi ya Miami ni mara baada ya kupata ushindi dhidi ya Mromania Simona Halep.

Katika mchezo huo, Konta alipoteza katika seti ya kwanza kwa 3-6 na baaadae akarejea mchezoni na kushinda katika seti ya pili kwa 7-6 (9-7) na kasha kupata 6-2 katika seti ya mwisho.

Mara baada ya kukamilika kwa mchezo huo Konta amesema ameshukuru sana kwa ushindi alioupata kwani mpinzani wake alionesha kiwango kizuri na kumpa ushindani mkali sana lakini sasa anajipanga kwaajili ya mchezo unaofata ambao anaamini utakuwa mgumu zaidi.

Kutokana na matokeo hayo, Konta atakutana na kati ya Venus Williams au Angelique Kerber.

Mchezo mwingine wa nusu fainali utakuwa ni kati ya Caroline Wozniacki na Karolina Pliskova.

Kwa upande wa wanaume Fabio Fognini kutoka nchini Italia amemshinda Kei Nishikori kutoka nchini Japankwa kupata ushindi katika seti mbili za moja kwa moja.

Katika seti ya kwanza Fabio alipata 6-4 na katika seti ya pili akapata 6-2 na kufanikiwa kuwa mchezaji wakwanza ambae hayupo katika wachezaji kumi bora kufanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali katika michuano ya wazi ya Miami.


Kwa upande wa wachezaji wawili kwa wanaume, Jamie Murray pamoja na mshirika wake Bruno Soares wametolewa katika michuano hiyo mara baada ya kupoteza katika seti ya pili kwa 6-3, na seti ya tatu kwa 10-8, katika seti ya kwanza jammie pamoja na mshirika wake walishinda kwa 6-2.

0 comments:

Post a Comment