Saturday, March 18, 2017

Kwenye interview na Sammisago kupitia FridayNiteLive Baraka Da Prince amesema hajawahi kuthibitisha popote kuwa Najma ana ujauzito wake.

Mwanzoni mwa mwaka 2017 palikuwa na taarifa za Najma kuwa na ujauzito wa Baraka na kwamba baada ya kwenda kwa wazazi wake Uingereza mimba hio ikapotea ghafla…..
Baraka anasema “Sijawahi kuthibitisha popote kuwa Najma anamimba, hii stori ilitokana na picha aliyoweka mtandaoni wakati ameongezeka kilo kidogo, nilimwambia toa hio picha sababu italeta stori kama hizi, pia sidhani kama wazazi wake wanaweza kukubali afanye kitu kama kutoa mimba“…
Baraka Da Prince alikuwa #FridayNiteLive akitambulisha video ya wimbo wake mpya #AchaNiende

0 comments:

Post a Comment