Wednesday, March 1, 2017

Kama umekuwa ukimfuatilia Harmonize kuanzia kwenye interviews ambazo anafanya mpaka kwenye pages zake za mitandao ya kijamii naamini utakuwa umegundua kuwa mkali huyo sio mkali sana katika suala zima la Lugha ya Kiingereza.

Pamoja na comments chafu ambazo Harmonize huwa anakutana nazo kutokana na tatizo hilo la Lugha mkali huyo ametusanua kwamba comments hizo hazimnyimi kabisa usingizi ispokuwa sasa hivi yuko katika mikakati ya kujifunza na kuhakikisha anaijua vizuri lugha hiyo.
“Niko najifunza, unajua watu wanashindwa kuelewa kitu kimoja, kila kitu ni hatua, hasa kwa sisi ambao tulikosa elimu bora. Sasa hutakiwi ku-concentrate sana na comments za instagram kwasababu kila mtu anakuwa na ubongo wake na akili yake, kuna mtu kaamka vibaya kakosa kazi ya kufanya na kuamua kuingia kwenye account na kutukana the way anajiskia. Ukisema uconcentrate na watu wanao comment vibaya mwisho wa siku utaanza kuwajibu watu.” Alisema Harmonize.

0 comments:

Post a Comment