Wednesday, March 1, 2017

Picha bado linaendelea, wiki iliyopita moja kati ya vitu ambavyo vilitrend kinoma noma ni pamoja na sauti iliyovuja zikisikika sauti za mchekeshaji Steve Nyerere pamoja na Mama mzazi wa muigizaji Wema Sepetu.

Sauti ambazo zilisikika zikijadili kuhusu mustakabali wa Wema Sepetu baada ya kudai kuchafuliwa na Chama cha Mapinduzi na hivyo kupanga mipango ya kuhamia chama pinzani cha CHADEMA.
Sauti ambazo zilizua gumzo kubwa hadi kupelekea Steve Nyerere kuitisha kikao na waandishi wa habari ili kulizungumzia suala hilo.
Shilawadu wametupenyezea ubuyu kwamba Steve Nyerere kumbe hakulipia ukumbi ambao alitumia kufanyia kukao hicho na waandishi wa habari na hivyo anatafutwa ili aweze kulipia gharama za kukodisha ukumbi huo.
Soudy Brown amemtafuta Steve Nyerere na kupiga nae story kuhusiana na suala hilo. Unataka kukijua ambacho alizungumza Steve!? Uhondo kamili nimekuwekea kwenye video hii hapa chini. Bonyeza play kusikiliza mwanzo hadi mwisho.

0 comments:

Post a Comment