Mwishoni mwa wiki iliyopita Diamond Platnumz aliweza kuizindua website yake ambayo inadeal na uuzaji wa kazi za wasanii kama nyimbo na vitu kama hivyo.
Ni hatua kwake Diamond Platnumz kuweza kufikiria na kufanya jambo hilo, ikiwa ni katika kulinda hatimiliki za kazi za wasanii na hata kuhakikisha msanii anapata anachostahili kutokana na malalamiko mengi kutokea hapo awali kuhusu wasanii kudhulumiwa haki zao.
Kila mmoja amempongeza Diamond Platnumz kwa hatua hiyo, Perfect Crispin alitaka kufahamu zaidi kuhusu hilo kuanzia kwenye faida hadi hasara zake.
Akaona sio kesi apige story na mkongwe, mtayarishaji wa muziki Bongo P Funk Majani katika kipindi cake cha On Point kinachoruka Clouds FM Jumapili saa 10 mpaka 12 jioni.
Majani amefunguka mtazamo wake kuanzia faida mpaka hasara ambazo yeye anafikiri zinaweza kutokea katika jambo kama hilo.
Nimekuwekea mazungumzo yote ya Perfect Crispin na P Funk Majani kwenye video hii hapa chini, bonyeza play ili uweze kusikiliza alichokiongea Majani mwanzo mpaka mwisho.
0 comments:
Post a Comment