Tuesday, March 14, 2017

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema mwaka 2016 ulikuwa mwaka mbaya kwa watoto nchini Syria, kwa kuwa mamia ya watoto waliuawa wakati watoto zaidi ya milioni sita nchini humo wakiishi kwa kutegemea misaada ya kibinadamu huku 250,000 wakikosa misaada hiyo.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirika hilo siku ya Jumatatu ya Machi 13, 2017, watoto 652 walikufa katika vita inayoendelea hadi sasa ambapo siku ya Jumatano itaingia mwaka sita.“Kiwango cha mateso kilikuwa kikubwa mno, kila mtoto atakuwa na makovu kwa maisha yake yote,” alisema Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa nchi za Mashariki ya Kati, Geert Cappelaere.
Aidha, ripoti hiyo inaeleza kuwa, ukosefu wa misaada ya kibinadamu pamoja na matibabu husababisha watoto wengi kupoteza maisha kwa sababu ya magonjwa yanayotibika au majeraha.
Kufuatia ugumu wa maisha uliyoikumba nchi hiyo, familia nyingi hulazimika kuchukua maamuzi makali, ikiwemo kuwapeleka watoto wao kwenye kazi ngumu au ndoa za utotoni.

0 comments:

Post a Comment