Bondia Hughie
Fury, ambae ni ndugu wa bondia Tyson Fury atapanda ulingoni May 6 mwaka huu
kuzichapa dhidi ya bondia Joseph Packer toka nchini New Zealand katika pambano
la ubingwa wa dunia WBO uzito wa juu.
Pambano hilo linataraji kuwa
kubwa na lenye kuvuta hisia za wengi kwani bondia Parker, 25, amekuwa bondia wa
kwanza mzaliwa wa New Zealand-mara baada ya kupata ushindi dhidi ya bondia Andy
Ruiz.
Hadi sasa bondia Hughie Fury ameshashuka
ulingoni na kushinda katika mapambano 22, kati ya mapambano hayo 18 akiwa
ameshinda kwa KO.
Kuelekea katika pambano hilo Fury
amesema anamheshimu sana Packer na anafahamu kuwa ni bondia mzuri sana lakini
atamshinda katika pambano hilo.
Akimzungumzia ndugu yake Tyson,
Fury amesema atahakikisha anashinda katika kila pambano ataloshuka ulingoni ili
ndugu yake atakapomaliza kutumikia adhabu yake wajipange kwa pamoja kuuteka
ulimwengu wa mchezo wa maumbwi.
Nae mwakilishi wa bondia packer toka
katika kampuni ya Duco Events David Higgins amesema mazungomzo yameshafika
pazuri baina ya pande zote mbili.
0 comments:
Post a Comment