Wednesday, March 22, 2017


Wanandinga wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania taifa Stars wameanza mazoezi katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam wakijiandaa dhidi ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Botswana Machi 25, 2017 na baadae kuivaa Burundi Machi 28.


Mazoezi hayo yamesimamiwa na Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga, na wasaidizi wake Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata, Meneja wa timu upande wa ufundi Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu na Daktari wa timuatakuwa Richard Yomba huku Daktari wa viungo   akiwa ni Gilbert Kigadya.




Wanandinga wa AStars ni walinda milango, Aishi Manula  (Azam FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe    (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).

Mayanga aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni   (Azam FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao     (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).

Kadhalika wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla  (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya    (Simba SC).

Viungo wa kushoto ni Farid Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui FC) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta      (KRC Genk- Ubelgiji), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu(Kagera Sugar) na Abdul-Rahman Mussa (Ruvu Shooting).

0 comments:

Post a Comment