Wednesday, March 8, 2017

 
Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, wanawake duniani kote huadhimisha siku yao ambapo hujitathmini kupitia shughuli mbalimbali za maendeleo walizofanya, changamoto zilizopo na kuweka mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo.


Wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakishiriki katika kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani,leo Jumatano Machi 8, 2017, ambapo jijini Dar es Salaam yalifanyika viwanja vya  mwembe yanga Wilayani Temeke.
Katika maadhimisho hayo ya siku ya Wanawake Duniani Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva, ambaye alimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye awali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ilisema Mkuu huyo wa Mkoa ndiye angekuwa mgeni rasmi lakini hakutokea.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mh Felix Lyaviva, (kushoto), akiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam


Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa wamebeba bango lenye maneno yasemayo "Tanzania ya viwanda: Msingi mkuu wa PPF kwa ajira za wanawake na maendeleo yao kiuchumi"



Pia kulikuwa na burudani mbalimbali na michezo ya jadi ambayo ilikuwa na dhima ya kumuinua mwanamke ajione kuwa anaweza.



Baadhi ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwa katika picha ya pamoja

 Wanawake watakiwa kujiunga na PPF

WANAWAKE nchini wametakiwa kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.

Wito huo ulitolewa na Janet Ezekiel Afisa Uhusiano Mwandamizi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Dunia.

Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa ni "Tanzania ya viwanda, Wanawake ndio Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi". 

0 comments:

Post a Comment